Ajenda ya Urekebishaji wa Sera ya Ardhi Nchini Kenya | Land Portal
Ajenda ya Urekebishaji wa Sera ya Ardhi Nchini Kenya
PDF icon Download file (360.73 KB)

Resource information

Date of publication: 
February 2019
Resource Language: 
Pages: 
6

Webinaa kuhusu Urekebishaji wa Sera ya Ardhi Nchini Kenya ilifanyika tarehe 10 Oktoba, 2018. Webinaa ilipitia mchakato wa urekebishaji wa Sera ya Ardhi nchini Kenya na ikashughulikia changamoto anuwai. Lengo lilikuwa  kubaini hatua za kufuata zitakazoleta usawa na haki katika urekebishaji wa sera ya ardhi.
Webinaa ilishughulikia maswali yafuatayo: 
Tumefika wapi katika mchakato wa urekebishaji wa Sera ya Ardhi?
Changamoto kuu zinazohitaji kushughulikiwa katika mfumo wa urekebishaji wa Sera ya Ardhi na matumizi ya ardhi ni zipi?
Umuhimu wa jinsia katika urekebishaji wa Sera ya Ardhi unaweza kufanikishwa  kwa namna gani?
Athari za kuuza ardhi ya jamii ni zipi?
Uhifadhi wa data kidijitali unashughulikia kwa namna ukinzani uliopo katika ofisi zinazohusika na rekodi za ardhi?
Webinaa iliandaliwa kwa ushirikiano wa Kenya Land Alliance (KLA), Serikali ya Kenya, Wakfu wa Tovuti ya Ardhi, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, na Muungano wa Uropa.
Msimamizi: Michael Ochieng Odhiambo, Director of People, Land and Rural Development (PLRD) 
Wanajopo:
Dkt. Collins Odote Oloo, Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Nairobi
Odenda Lumumba, Afisa Mkuu, Shirika la Masuala ya Ardhi Nchini Kenya (KLA).
Husna Mbarak, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) 
Watu 132 walijisajili kwa webinaa na  hatimaye watu 58 walishiriki. 
Video kamili ya webinaa hiyo inapatikana katika YouTube:  https://youtu.be/IDGEpHrK95U

Authors and Publishers

Publisher(s): 

European Commission


The European Commission represents the general interest of the EU and is the driving force in proposing legislation (to Parliament and the Council), administering and implementing EU policies, enforcing EU law (jointly with the Court of Justice) and negotiating in the international arena.

Share this page